Mwanamke apoteza pua kwa uraibu wa kokeini

By Zanura Mollel , Nipashe
Published at 06:19 PM Sep 30 2025
@nipashedigital

Kelly, mwanamke kutoka Marekani, amesimulia kwa uchungu safari yake ya uraibu wa dawa za kulevya uliomgharimu afya na heshima ya mwonekano wake, baada ya kupoteza kabisa sehemu ya pua yake. Katika video iliyosambaa mitandaoni, Kelly alieleza kuwa alianza kutumia kokeini kila siku kwa miaka miwili baada ya kufiwa na mume wake. Anasema mshtuko na huzuni ya kifo hicho vilimfanya apoteze matumaini na hatimaye kuangukia kwenye uraibu. Kabla ya msiba huo, wawili hao walikuwa wakikabiliana na changamoto ya unywaji pombe kupita kiasi. Baadaye mume wake alifanyiwa upasuaji na kuandikiwa dawa za maumivu aina ya opioids, ambazo zilipelekea utegemezi mkubwa. Hatimaye alifariki dunia kutokana na dozi kubwa isiyokusudiwa. “Nilipokuwa nikiomboleza kifo cha mume wangu, hakuna kitu nilichokijali tena,” alisema Kelly kwa majonzi. Uamuzi wake wa kujifariji kwa kokeini ulimgeukia janga, kwani afya yake ilianza kudhoofika kwa kasi. Pua yake ilianza kuharibika hatua kwa hatua na hatimaye ikaanguka kabisa. Awali, alidhani jeraha hilo lingepona pindi angeacha dawa hizo, lakini hali ilizidi kuwa mbaya zaidi. Alieleza kuwa maumivu aliyoyapitia yalikuwa makali mno, na ilimbidi afanyiwe upasuaji mara 15 kujaribu kuijenga upya pua yake. Katika moja ya upasuaji huo, madaktari walichukua kipande cha ngozi kutoka kichwani na kukipandikiza kwenye pua. “Huenda sitaishi ndani ya pua yangu tena milele,” alisema kwa uchungu, akifafanua alama ya kudumu iliyobaki maishani mwake. Hata hivyo, Kelly sasa ameanza ukurasa mpya. Amekuwa msafi bila kutumia dawa za kulevya kwa zaidi ya miaka minne, na amegeuza simulizi yake kuwa fundisho kwa wengine, akiwatahadharisha waepuke kokeini na dawa nyingine za kulevya. Imeandikwa na Zanura Mollel Tembelea http://epaper.ippmedia.com kusoma gazeti lako au wasiliana nasi 📞+255 745 -700 710 au 0677- 020 701 kwa maelezo zaidi. #NipasheDigital #NipasheMwangaWaJamii #miaka30yakupashahabari

♬ original sound - Nipashe Digital
Mwanamke apoteza pua kwa uraibu wa kokeini.

Kelly, mwanamke kutoka Marekani, amesimulia kwa uchungu safari yake ya uraibu wa dawa za kulevya uliomgharimu afya na heshima ya mwonekano wake, baada ya kupoteza kabisa sehemu ya pua yake.

Katika video iliyosambaa mitandaoni, Kelly alieleza kuwa alianza kutumia kokeini kila siku kwa miaka miwili baada ya kufiwa na mume wake. Anasema mshtuko na huzuni ya kifo hicho vilimfanya apoteze matumaini na hatimaye kuangukia kwenye uraibu.

Kabla ya msiba huo, wawili hao walikuwa wakikabiliana na changamoto ya unywaji pombe kupita kiasi. Baadaye mume wake alifanyiwa upasuaji na kuandikiwa dawa za maumivu aina ya opioids, ambazo zilipelekea utegemezi mkubwa. Hatimaye alifariki dunia kutokana na dozi kubwa isiyokusudiwa.

“Nilipokuwa nikiomboleza kifo cha mume wangu, hakuna kitu nilichokijali tena,” alisema Kelly kwa majonzi. Uamuzi wake wa kujifariji kwa kokeini ulimgeukia janga, kwani afya yake ilianza kudhoofika kwa kasi. Pua yake ilianza kuharibika hatua kwa hatua na hatimaye ikaanguka kabisa.

Awali, alidhani jeraha hilo lingepona pindi angeacha dawa hizo, lakini hali ilizidi kuwa mbaya zaidi. Alieleza kuwa maumivu aliyoyapitia yalikuwa makali mno, na ilimbidi afanyiwe upasuaji mara 15 kujaribu kuijenga upya pua yake. Katika moja ya upasuaji huo, madaktari walichukua kipande cha ngozi kutoka kichwani na kukipandikiza kwenye pua.

“Huenda sitaishi ndani ya pua yangu tena milele,” alisema kwa uchungu, akifafanua alama ya kudumu iliyobaki maishani mwake.

Hata hivyo, Kelly sasa ameanza ukurasa mpya. Amekuwa msafi bila kutumia dawa za kulevya kwa zaidi ya miaka minne, na amegeuza simulizi yake kuwa fundisho kwa wengine, akiwatahadharisha waepuke kokeini na dawa nyingine za kulevya.