Waziri Mkuu, Dk.Mwigulu Nchemba, amemwagiza Kamishna wa Uhamiaji nchini kukamata hati ya kusafiria (passport) ya Mkandarasi wa Kampuni ya Impresa Di Construzioni Ing E. Mantovani ya nchini Italia ili asitoke nje ya nchi kutokana na kushindwa kukamilisha ujenzi wa mradi wa Kituo cha Pamoja cha Ukaguzi wa Magari (One Stop center) kilichopo kata ya Mhalala wilayani Manyoni mkoani Singida.
Ametoa agizo hilo leo Novemba 21, 2025 baada ya kukagua ujenzi wa mradi huo ambao una thamani ya Euro 9,537,607.90 sawa na zaidi ya Sh. bilioni 26 za kitanzania ambao ulitakiwa kukamilika 2018 lakini umesimama tangu 2016 hadi sasa baada ya mkandarasi huyo kutangaza nchini kwao Italia kwamba amefilisika.
“Kwa taarifa nilizonazo alitangaza kwamba amefilisika kule kwao Italia na kwamba hawezi kuendelea na mradi, hata hivyo mahakama ya Italia ikaelekeza mkandarasi ailipe Tanzania kwasababu amechelewesha mradi, chakushangaza zikaanza ngonjelangonjela,” amesema.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED