Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, amevunja ukimya kuhusu uvumi unaoenezwa na baadhi ya watu kwamba mabasi ya kampuni ya Ester ni mali yake akisema jambo hilo sio la kweli na kuwataka Watanzania kutokubali kila wanachoelezwa.
“Siku hizi watu hawaogopi hata kusingizia jambo unakuta mtu hafanyi hata utafiti juu ya mtu anayetaka kumsema, juzi juzi nikasikia tumechoma magari ya Ester ya mbunge wa Iramba Magharibi, magari yake yanaitwa Ester ameyaita Ester jina la mke wake,”…
“Mke wangu mimi haitwi Ester anaitwa Neema, wanasema basi kama sio ya mke wake yatakuwa ya mama yake mama yangu binti wa kiislamu anaitwa Asha Ramadhani Mohamed,”
Dk.Mwigulu ambaye ametoa ufafanuzi huo leo (Novemba 21, 2025 wakati akizungumza na mamia ya wananchi kwenye viwanja vya Bombadia Manispaa ya Singida, amesema yeye amezaliwa katika familia ya kifugaji ambayo huruhusiwi hata kufanya biashara ya miwa hivyo hajawahi kufanya biashara yeyote.
“Nimeingia huku serikalini uwekezaji mkubwa ninaoufanya ni kusomesha watoto na nina kundi la watoto zaidi ya 500 ninaowasomesha, nimewekeza kwenye huduma za watu,”amesema Dk.Mwigulu.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED