IGP Wambura: Siasa, dini visitugawe Watanzania

By Godfrey Mushi , Nipashe
Published at 03:50 PM Nov 21 2025
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Camillus Wambura.
Picha:Mpigapicha Wetu
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Camillus Wambura.

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Camillus Wambura, amewapa 'somo' Watanzania, akiwataka wasikubali kugawanyika kutokana na sababu yeyote ile, iwe ya kisiasa, kidini au rasilimali.

Aidha, amewaomba Watanzania washirikiane na Polisi popote, kuhakikisha nchi inakuwa salama.

Wambura, ameeleza hayo leo Novemba 21,2025 katika Shule ya Polisi Tanzania (TPS) iliyopo Moshi, mkoani Kilimanjaro, alipokwenda kufunga mafunzo ya awali ya Polisi, kozi namba 01 ya mwaka 2024/2025.

Askari wapya 4,826 wakiwamo wanaume 3,436 na wanawake 1,390, wamehitimu mafunzo hayo.

 â€œTusikubali kugawanyika kutokana na sababu yeyote ile iwe ya kisiasa, kidini au rasilimali. Tuendelee kutunza tunu yetu ya usalama na amani ya nchi yetu iliyodumu takribani kwa miongo mingi sasa.Tushirikiane popote kuhakikisha tunakuwa salama.

Aidha, Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi amewaonya askari wapya akisema: “Kamwe msijemkajiingiza katika utendaji wa kimazoea usiozingatia sheria kanuni na taratibu, mkaendeleze tabia ya kujifunza zaidi maishani mwenu, ili mjijengee weledi na uwezo wa kiutendaji kulingana na mahitaji ya sayansi na teknolojia.