Tunalaani vurugu za Oktoba 29

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 09:29 AM Nov 21 2025
Tunalaani vurugu za Oktoba 29

Taasisi na Jumuiya za Kiislamu na Baraza la Waislamu Tanzania, (BAKWATA), zimelaani matukio ya vurugu yaliyotokea Oktoba 29, 2025 na kusababisha vifo vya watu, uharibifu wa mali za watu binafsi, miundombinu ya umma na kuathiri taswira ya nchi.

Kutokana na matukio hayo, amesema kumekuwepo na matamko yanayolenga maridhiano na hatimaye kuirejesha amani na yale yanayochochea kuendelea kwa vurugu, hivyo muhimu kumuomba Mungu ili amani itawale.

"Sisi tunalaani matukio haya na tumesikitishwa sana na vifo vilivyotokea, uharibifu wa mali za watu binafsi na miundombinu ya umma na imeathiri taswira ya nchi yetu," amesema.

Kauli hiyo imetolewa, Alhamisi Novemba 20, 2025 na Amiri wa Baraza Kuu na Jumuiya za Taasisi hizo, Sheikh Mussa Kundecha alipozungumza na wanahabari, jijini Dar es Salaam.