Hatimaye, mwili wa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais (Mstaafu), Hayati Cleopa David Msuya, umefikishwa leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) majira ya saa 2:22 asubuhi.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Nurdin Babu, mwili wa Hayati Msuya utapitishwa kwa mwendo wa taratibu kupitia barabara ya Arusha–Moshi, kuelekea viwanja vya CD Msuya vilivyopo wilayani Mwanga, mkoani Kilimanjaro.
Amesema kuwa maandalizi yamekamilika ili kutoa fursa kwa wananchi mbalimbali kushiriki na kutoa heshima za mwisho kwa kiongozi huyo wa kihistoria. Viwanja hivyo vinakadiriwa kuwa na uwezo wa kuchukua zaidi ya watu 15,000 kwa wakati mmoja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuongoza shughuli za maziko ya Hayati Cleopa Msuya.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED