Nitaongoza nchi bila Kukopa mikopo nje-Doyo

By Thobias Mwanakatwe , Nipashe
Published at 08:10 PM Oct 01 2025
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha NLD, Doyo Hassan Doyo.
Picha: Mpigapicha Wetu
Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha NLD, Doyo Hassan Doyo.

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha NLD, Doyo Hassan Doyo, amesema iwapo wananchi watakipa ridhaa chama hicho serikali yake itaongoza nchi kwa kutumia raslimali zilizopo nchini na sio kukopa mikopo kutoka nje.

Akizungumza na wananchi wa Manispaa ya Singida leo (Oktoba 1, 2025) kwenye eneo la Soko Kuu la Singida, amesema ni aibu kwa nchi kukopa wakati kuna raslimali za kutosha kama madini na maliasili ambazo zikitumika vizuri zinaweza kuongoza nchi pasipo kutegemea mikopo kutoka nje.

“Nikiwa rais nitaendesha nchi kwa raslimali zilizopo sio kwa mikopo nitatumia madini kama dhahabu,tanzanite,maliasili zilizopo kuwaongoza watanzania hatutaenda kukopa,raslimali zilizopo nchi hii kukopa ni aibu, nakwenda kuongoza serikali isiyokuwa na madeni na madeni yaliyokopwa kupitia sekta ya madini nitakwenda kuyalipa katika kipindi changu cha miaka mitano,”amesema.