Rais Dk Mwinyi aongeza ukomo wa Baraza la Wawakilishi hadi Agosti 13

By Rahma Suleiman , Nipashe
Published at 01:49 PM Jun 23 2025
Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi
Picha: Mpigapicha Wetu
Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi

Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameongeza ukomo wa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi hadi Agosti 13 mwaka huu.

Dk. Mwinyi alitoa kauli hiyo leo, Juni 23,2025 wakati akihutubia hotuba ya kulifunga baraza hilo huko Chukwani, Zanzibar, ambapo alisema ukomo wa Baraza la 10 utafikia Agosti 13 mwaka huu, kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar.

Amesema kwa mujibu wa Kifungu cha 91(2)(a) cha Sheria ya Zanzibar ya mwaka 1984, anayo mamlaka ya kuongeza muda wa Baraza hilo.

Baraza hilo la 10 lilifunguliwa rasmi na Rais Dk. Mwinyi Novemba 11, 2020, baada ya kuingia madarakani.

Baraza hilo linaundwa na wajumbe kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), ACT Wazalendo na mjumbe mmoja kutoka Chama cha ADA-TADEA.