CCM yajigamba Dodoma itabaki kuwa ngome yao

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 07:03 PM Jun 23 2025
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, Amos Makalla.
Picha:Mpigapicha Wetu
Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, Amos Makalla.

Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Taifa, Amos Makalla, amesema Dodoma zikiwamo Mpwapwa na Kongwa ni ngome ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Ameyasema hayo leo Juni 23, 2025, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Mpwapwa mjini, mkoani Dodoma, wakati wa ziara yake ya siku tatu aliyoianza ikihusisha mkoa huo na Singida.

Amewaeleza wananchi  kama walivyokiamini chama hicho kwa kukipa ushindi wa asilimia 98 katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ifikapo mwezi Oktoba wakatiki tena kwa kishindo.

Makalla amesisitiza kuwa hao wanaosema No Reforms No Election wasiwadanganye Watanzania, wamepumzika baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuwafilisi ajenda zao zote.

“Akija mtu hapa akawaambia barabara kutoka Mpwapwa - Kongwa mbovu, mwambie Samia ametiki barabara itajengwa. Ajenda zao nyingi haziko wamefilisiwa sasa wameamua kupumzika,” amesema.