Majaliwa atoa maagizo saba kwa taasisi za umma

By Paul Mabeja , Nipashe
Published at 06:42 PM Jun 23 2025
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Picha: Mpigapicha Wetu
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ametoa maagizo saba ikiwemo kupatiwa taarifa ya taasisi zote za umma ambazo zitakua bado hazijajiunga na mfumo wa pamoja unaowezesha mifumo mbalimbali ya serikali kuwasiliana na kubadilishana taarifa (GovESG) hadi Julai 30, 2025 ili zitoe maelezo kwanini hazijateleza takwa hilo la kisheria.


Majaliwa, amesema hayo leo Juni 23, 2025 jijini Dodoma, wakati akifunga maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma pamoja na uzinduzi wa mifumo ya kidijitali itakayo tumiwa na taasisi za umma.

“Taasisi zote za umma ambazo hazijajiunga na mfumo huu mwisho ni Julai 30, 2025 wote mnapaswa kuwa mmeshaingia pale GovESG, huu ni msisitizo uliotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa lazima utakapo kamilika taasisi zote zijiunge ili mifumo indelee kusoma na kutoa taarifa,”amesisitiza Majaliwa

Aidha, Majaliwa amesema takwimu zinaonyesha kuwa hadi sasa idadi ya taasisi zilizounganishwa ni ndogo ukilinganisha na zilizopo ndani ya serikali.