Rais Samia: Mchakato Katiba Mpya kuanza ndani ya Siku 100

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 11:07 AM Aug 29 2025
Mgombea urais CCM, Samia Suluhu Hassan

Mgombea urais CCM, Samia Suluhu Hassan, amesema ndani ya siku 100 za mwanzo akipewa ridhaa ya kuongeza nchi, kupitia Falsafa ya R4 wataendelea mashauriano na wadau wa siasa, taasisi za kiraia na sekta za binafsi kwa kuunda tume ya kuanzisha mazungumzo ya maridhiano na upatanishi na kuandaa mazingira ya kuanza mchakato wa Katiba Mpya.