Pingamizi la Esther Matiko dhidi ya mgombea ACT Tarime Mjini latupwa

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:47 PM Aug 29 2025
Pingamizi la Esther Matiko dhidi ya mgombea ACT Tarime Mjini latupwa
Picha:Mpigapicha Wetu
Pingamizi la Esther Matiko dhidi ya mgombea ACT Tarime Mjini latupwa

Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Tarime Mjini, Erasto Mbunga, ametupilia mbali pingamizi lililowekwa dhidi ya mgombea ubunge kupitia Chama cha ACT Wazalendo, Kangoye Jackson.

Pingamizi hilo liliwasilishwa na mgombea ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Esther Matiko, aliyedai kuwa Kangoye alijiunga na ACT Wazalendo kinyume na taratibu, akibainisha kuwa aliingia chama hicho kabla ya kutimiza siku saba tangu kuondoka CCM, na baada ya mchakato wa ndani wa chama hicho kukamilika.

Hata hivyo, baada ya kupitia hoja hizo, msimamizi wa uchaguzi alitupilia mbali pingamizi hilo na kumruhusu Kangoye kuendelea na mchakato wa kugombea ubunge kupitia ACT Wazalendo katika uchaguzi huo.

Katika vielelezo vilivyowasilishwa, ilionekana pia ushiriki wa viongozi wa ACT Wazalendo wakiwemo Charles Mwera, Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mara, pamoja na Ibrahim Juma, Katibu wa ACT Wazalendo Wilaya ya Tarime, waliothibitisha usajili na uhalali wa Kangoye ndani ya chama.