Dk. Samia aahidi kuimarisha Utalii Morogoro

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 07:14 PM Aug 29 2025
Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan.

Mgombea Urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan, amedhamilia kuifungua Morogoro kiutali ili kuvutia mikutano na shughuli mbalimbali zitakazowanufaisha na kukuza uchumi wa wananchi wa mkoa huo.

Dk Samia ambaye ni Rais wa Tanzania amesema hayo leo Ijumaa wakati akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika manispaa ya Morogoro, katika mwendelezo wa kampeni za kujinadi ili kusaka kura kwa Watanzania.

Mkuu huyo wa nchi, amesema tayari maandalizi yameshaanza ikiwemo ukalimishwaji wa ujenzi wa reli ya kisasa SGR ambapo barabara ya itakayojengwa kutoka stesheni ya reli hadi hifadhi ya Taifa ya Mikumi itakuza utalii.

“Lakini kabla ya ujenzi wa barabara hiyo, kwa kiasi fulani utalii ndani ya Morogoro umeongezeka.Lakini tutajnga kituo kikubwa na cha kisasa mikutano katika eneo ambalo mkoa utatupangia,”

“Tunataka watu wengi zaidi waje kutembea Morogoro, kibiashara na kiutalii katika mbuga zilizopo.Jitihada zote zitaongeza fursa za ajira kwa wananchi wetu na kuimarisha huduma za makazi za mkoa wa Morogoro,”ameeleza Dk Samia.