Rais Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Baraza Kuu la Idd la kitaifa, litakalofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNCCI) jijini Dar es Salaam.
Taarifa hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Omari Alhad Walid, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwa niaba ya Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuberi.
Kwa mujibu wa Sheikh Walid, Baraza hilo linatarajiwa kufanyika kati ya Machi 31 au Aprili 1, 2025, kulingana na muandamo wa mwezi.
Wakati huohuo, Sheikh Walid ametangaza kuwa Swala ya Idd Kitaifa ya mwaka 1446 Hijria (2025) itafanyika jijini Dar es Salaam, katika Msikiti wa Mfalme wa Sita (King Faisal Mosque), uliopo katika Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).
Aidha, amewataka Watanzania kudumisha utulivu, hekima na mshikamano katika kipindi cha kuelekea Sikukuu ya Idd, kama ilivyo katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED