Chama cha Sauti ya Umma (SAU), kimevuna wanachama tisa kutoka CCM, katika mkutano wake wa hadhara ulipfanyika mjini Shinyanga leo asubuhi.
Wanachama hao walijiunga na chama hicho, katika mkutano uliohutubiwa na mgombea urais Majalio Kyara ambaye akikabidhi ya SAU kwa mmoja wao aliyejitambulisha kwa jina la Robert Khamis.
Akikabidhi kadi ya CCM na kupokea mpya ya SAU, Khamis amesema amejiunga na chama hicho baada ya kuridhika na ahadi za mgómbea huyo.
"Mheshimiwa mgómbea urais, tumefurahishwa na ahadi zako kuhusu kutoa huduma za afya bure, tunateseka sana kutafuta huduma hiyo," amesema Khamis.
Amesema wananchi wengi wanakosa matibabu kwa sababu hawana fedha, na kwamba ahadi ya SAU imewapa matumaini mapya ndio maana wamehamia katika chama hicho.
"Mheshimiwa rais mtarajiwa ukiingia ikulu ulichukulie kwa uzito suala la afya za Watanzania, huku kwetu ni shida, huduma za afya zina gharama kubwa," amesema.
Mgómbea urais wa chama hicho, Majalio Kyara, amesema SAU ikiingira madarakani itafanya mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali ikiwamo ya afya ili kuboresha maisha ya Watanzania.
"Mtuunge katika kampeni zetu ili tufanye mabadiliko mbalimbali yanayoendana na wakati wa sasa. Tutaondoa kila aina ya urasimu, Watanzania wapate zinazostahili," amesema Kyara.
Mgómbea huyo na timu yake wameelekea mkoani kuendelea na kampeni ambazo zitawafikisha hadi mkoa na Kigoma.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED