“Serikali ya CHAUMMA itasaidia mawazo ya kibiashara ya vijana”

By Elizabeth Zaya , Nipashe
Published at 08:14 PM Sep 16 2025
Mgombea Urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu.

Mgombea Urais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Salum Mwalimu, amesema serikali yake itaanzisha mfuko maalumu kwa ajili ya kusaidia, kusimamia na kuendeleza mawazo ya kibiashara ya vijana nchini.

Akizungumza leo mjini Geita katika mkutano wa kampeni, Mwalimu alisema lengo ni kuhakikisha hakuna biashara ya kijana inayokufa chini ya uongozi wake.

Ameongeza kuwa serikali yake itashirikiana na wawekezaji kutengeneza mfuko maalumu wa kuratibu na kusimamia matumizi ya mapato ya Mfuko wa Jamii wa Makampuni Makubwa (CSR), ili fedha hizo zisitumike vibaya.