Simanzi kuagwa mwili wa Shyrose, serikali yaagiza wauaji wasakwe usiku na mchana

By Nebart Msokwa , Nipashe
Published at 04:48 AM Sep 21 2025
“Tukio hili ni la aibu sana kwetu wana Mbeya, waliofanya tukio hili ni watoto wetu, ni ndugu zetu na ni wenzetu, kwahiyo kila mmoja wetu anao wajibu wa kukemea matukio haya,”

Hali ya simanzi imetawala nyumbani kwa Dk. Mabula Mahande mkazi wa Uzunguni jijini Mbeya wakati wa kuaga mwili wa mwanaye, Shyrose Mahande (21) ambaye alitekwa na watu wasiojulikana na kuuawa kisha mwili wake kuchomwa moto.