SIKU moja baada ya Mkoa wa Tanga, kupendekeza kugawanywa kwa majimbo ya Handeni, Kilindi na Muheza, baadhi ya wanasiasa, kikiwemo Chama Makini kimeibua hoja kinzani kwamba, mkakati huo huenda unalenga kupima upepo wa kisiasa.
Mwenyekiti wa Chama cha Makini, Mkoa wa Tanga, Assely Shewally, amesema ugawaji wa majimbo hayo, umejikita zaidi katika matamanio ya kisiasa kuliko uhalisia wa mgawanyo; kutokana na sababu za madaraka na kupata nafasi ya ubunge.
Shewally ameyasema hayo leo, wakati akizungumza na Nipashe Digital kuhusu mchakato unaoendelea nchini wa kupendekeza mgawanyo wa majimbo unaofanywa na Kamati za Ushauri wa Mikoa (RCC).
Amesema ugawaji wa majimbo mara nyingi umekuwa hauleti tija kwa maendeleo ya nchi kwa sababu kasi ya uchumi imezidi kupungua kutokana na kuongeza gharama.
Mkuu wa Mkoa huo, Balozi Dk. Batilda Burian, amethibitisha kuwa Jimbo la Kilindi, linapaswa kugawanywa kwa sababu ya kukidhi vigezo vya idadi ya watu, huku Handeni nayo ikifikia vigezo kama hivyo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED