PEMBEZONI mwa Mkutano wa Mpango wa Mattei kwa Afrika na ‘EU Global Gateway’ jijini Roma, Italia, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi, Mahmoud Thabit Kombo;
Amekutana na Waziri wa Ulinzi wa Tanzania, Stergomena Tax aliyekuwa kwenye ziara ya kikazi nchini humo, Tanzania na Italia zimesaini Hati ya Ushirikiano katika Masuala ya Ulinzi.
Kwa pamoja viongozi hao walifanya kikao cha pamoja na watumishi wa wizara walioambatana nao, watumishi na watendaji wa Ubalozi wa Tanzania nchini Italia pamoja na wawakilishi wa Diaspora ya Watanzania waishio Italia.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED