Tusitengenezeane ajali sehemu za kazi - RC Simiyu

By Maulid Mmbaga , Nipashe
Published at 12:33 PM May 02 2025
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kenani Kihongosi.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenani Kihongosi amewasisitiza viongozi na watumishi kutotengenezeana ajali katika maeneo yao ya kazi kwani hupunguza ufanisi katika utendaji wa kazi.

Kihongosi, ameyasema hayo alipokuwa Mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Mei Mosi wilayani Maswa mkoani Simiyu ambapo tukio hilo limefanyika kimkoa.

Kihongosi amesisitiza watumishi kushirikiana na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan na kusimamia haki kama Rais alivyoelekeza.

Mwisho amewasisitiza watumishi kuzidi kulinda amani na utulivu na kutoruhusu vurugu za aina yoyote kutokea katika maeneo yao kwani Amani ndio Msingi wa Maendeleo ya Taifa.