UWAMWA kunusuru wanafunzi na adha ya usafiri

By Elisante John , Nipashe
Published at 02:03 PM Jun 25 2025
Katibu tawala mkoa wa Mwanza Balandya Elikana akikata utepe kuaashiri uzinduzi wa gari kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi kwa kutumia kadi, (kushoto kwake) ni Mwenyekiti wa ushirika wa usafirishaji mkoa wa Mwanza (UWAMWA) Jabir Magera.
PICHA:ELIZABETH FAUSTINE
Katibu tawala mkoa wa Mwanza Balandya Elikana akikata utepe kuaashiri uzinduzi wa gari kwa ajili ya kusafirisha wanafunzi kwa kutumia kadi, (kushoto kwake) ni Mwenyekiti wa ushirika wa usafirishaji mkoa wa Mwanza (UWAMWA) Jabir Magera.

Ushirika wa usafirishaji mkoa wa Mwanza UWAMWA imezindua gari 10 kwa lengo la kusafirisha wanafunzi kwenda shule na kuwarudisha ili kuepuka adha wanazopata katika usafiri wa umma.

Akieleza mpango huo Mwenyekiti wa Ushirika wa usafirishaji Mkoa wa Mwanza UWAMWA Jabiri Magera, amesema wameboresha utoaji wa huduma ya usafirishaji wa wanafunzi kwa kuwa na mfumo tiketi mtandao na malipo ya kadi na kufanya mji wa Mwanza kwenda kwenye mifumo ya kisayansi.

"Tunagemea kutoa elimunzaidi kwa abiria ili wapokee mabadiliko haya kwa mtazamo chanya tunapoenda kutoa malipo ya pesa taslimu kwa kondakta mlangoni ili waanze kuzoea kwenda kwenye matumizi ya kadi lakini pia matumizi ya tiketi mtandao ili kusaidia jamii ambayo walikuwa wakilalamikia kwenye mambo mbalimbali ikiwemo ukatishaji wa 'ruti' na adha ya kupandishiwa nauli" amesema Magera


Akizindua gari hizo Katibu tawala Mkoa wa Mwanza Balandya Elikana amesema yote hayo ni matokeo ya ushirika ambayo huunganisha nguvu ya kuwaweka pamoja ili kurahisisha utoaji wa huduma.

"Tunazindua magari haya kwa ajili ya kuhudumia wanafunzi wetu katika shule za umma kwenye mkoa wa Mwanza na kwa leo tunaanza kwa kuzindua magari 10 lakini kadri shughuli itakavyokuwa inaboreka magari yatazidi kuongezwa ili kukidhi haja ya mahitaji ya wanafunzi wetu wa shule za umma mkoani Mwanza hasa kwenye manispaa ya Ilemela hivyo tuendelee kuuboresha huu ushirika wetu" amesema Elikana


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa Ardhini (LATRA) Johansen Kahatano,  amesema wametoa elimu ya ushirika mkoani Mwanza kwa zaidi ya miaka mitatu sasa na kwamba  tayari wamekabidhi cheti cha wakala wa wakutoa leseni ushirika wa usafirishaji mkoa wa Mwanza UWAMWA  ilikutoa huduma.

"UWAMWA wamefika mbali zaidi kwa kununua mabasi haya ambayo watayatumia kwa ajili ya kubeba wanafunzi  na tunapoelekea sasa ni kuwapa njia maalum ya kuwa wenyewe ambayo wataitumia wao, tunaamini kwa kufanya hivyo wataweza kuongeza mapato yao" amesema Kahatano