EWURA yaitaka DAWASA kuimarisha huduma kwa wateja

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 08:40 PM Jun 25 2025
Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dk. James Mwainyekule.

Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Dk. James Mwainyekule, amewasitiza Maofisa Huduma kwa Wateja wa DAWASA kuendelea kuimarisha huduma kwa wateja wakati akifungua semina ya kutathmini hali ya huduma kwa wateja wa mamlaka, leo Juni 25,2025 Jjijini Dar es Salaam.

EWURA imechukua hatua hiyo kwa kuwa 27% ya malalamiko yanayohusu Mamlaka za Maji nchini kati ya mwaka 2023/24 na 2024/25 yaliihusu DAWASA na 60% ya malalamiko hayo yanahusu ankara za maji.

EWURA huzidhibiti kiufundi na kiychumi mamlaka za majisafi na usafi wa mazingira za miji mikuu ya mikoa, miji ya wilaya, miji midogo na miradi ya kitaifa.