Waandishi habari kuanza kusajiliwa Mei

By Vitus Audax , Nipashe
Published at 10:45 PM Mar 28 2025
Waandishi habari kuanza kusajiliwa Mei
Picha: Mpigapicha Wetu
Waandishi habari kuanza kusajiliwa Mei

BODI ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imesema inatarajia kuanza utaratibu wa kusajili waandishi wa habari kupitia mfumo wa kidijitali ifikapo mwanzoni mwa mwezi Mei, 2025.

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari leo na na bodi hiyo kwa kushirikiana na idara ya Habari Maelezo imeeleza kuwa ukamilishaji wa mfumo huo utakaotumika kwaajili ya usajili unaendelea kwa mafanikio.

Aidha taarifa hiyo iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa bodi  hiyo Patrick Kipangula imeeleza kuwa mfumo huo unatarajia kukamilika mwishoni mwa mwezi Aprili.

Kadhalika imeeleza kuwa baada ya kupokea maoni ya wadau mbalimbali yanayolenga kuimarisha zaidi uasalama, ubora, ufanisi na wenye kukidhi mahitaji imebidi kuongeza muda wa ukamilishaji wake.