WATAALAMU wa Afya Kanda ya Iringa wametakiwa kutunza na kulinda vifaa tiba katika hospitali na vituo vya kutolea huduma za afya ili viweze kudumu kwa muda mrefu.
Agizo hilo limetolewa leo na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Njombe, Joseph Mutashubirwa wakati kikao cha wadau wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Iringa chenye lengo la kujadili kwa pamoja na kuboresha uhimarishaji wa mnyororo wa bidhaa za afya kilichofanyika mjini Njombe.
Awali, Kaimu Meneja wa Bohari ya Dawa (MSD) Kanda ya Iringa, Lucas Guta amesema wameona ni vema wakakaa na wadau na kuzungumza juu ya huduma wanazozitoa kama zinakidhi mahitaji yao au hazikidhi ili kuweza kuzifanyia kazi.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED