VIJANA wakubwa barani Ulaya walirejea katika michuano ya bara wiki iliyopita huku mechi zote nane za hatua ya 16-bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya zikipigwa.
Liverpool, Arsenal na Aston Villa zilikuwa timu za England zilizofanya safari nzuri, huku watatu hao wakirejea nyumbani na ushindi kabla ya mechi ya mkondo wa pili wiki hii kwenye ardhi ya nyumbani.
Furaha haikuishia hapo, kulikuwa na dabi ya Madrid huko Santiago Bernabeu (Real Madrid dhidi ya Atletico Madri), vita vya wababe wa Ligi Kuu Ujerumani, Bundesliga, Bayern Munich na Bayer Leverkusen ilikuwa moto na Barcelona nao wakitakata mbele ya Benfica.
Hapa tunawaangalia wachezaji saba waliong'ara zaidi kwenye mechi hizo za mkondo wa kwanza wa hatua ya 16-bora ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
7. Vitinha (Paris Saint-Germain)
Paris Saint-Germain walipata pigo katika dakika ya 87 ya mechi yao Jumatano, huku nyota wa Liverpool, Harvey Elliott akikatiza matarajio yao ya robo fainali kwa kupata bao la dakika za mwisho.
PSG walikuwa na nguvu kubwa katika mchezo wa upande mmoja, na kuwakosesha pumzi Liverpool kwa muda mrefu kutokana na ufundi wao wa kumiliki mpira. Lakini nyota wa kireno, Vitinha alikuwa katikati ya ubora wake.
Alifurahia miguso 32 zaidi ya mchezaji mwingine yeyote uwanjani hapo, alikamilisha asilimia 96 ya pasi zake 114 alizojaribu na hata kutengeneza nafasi tatu kutoka kwenye nafasi ya chini-chini - Achraf Hakimi pekee ndiye aliyeweza kumkaribia kwa mbali.
6. Ethan Nwaneri (Arsenal)
Wakiwa wameambulia patupu katika mechi mfululizo, Arsenal walifanya fujo dhidi ya PSV Eindhoven Jumanne usiku. Walitoa kichapo cha mabao 7-1 dhidi ya timu ya kocha Peter Bosz na kiliwakumbusha washambuliaji waliokuwa na uwezo wao licha ya majeraha mengi katika idara ya ushambuliaji.
Ethan Nwaneri alikuwa mmoja wa wale walioingia katika ushindi mkubwa, kwa mara nyingine tena akiishi kulingana na lebo yake ya ajabu. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17, alionesha mchezo wa hali ya juu huku akiendelea kustaajabisha.
Alisimamia miguso mingi ya pamoja katika eneo la penalti la wapinzani huko Eindhoven na vile vile kusajili mikwaju mingi na juhudi kwenye goli kuliko mchezaji mwingine yeyote. Lilikuwa ni onesho lingine la kutia moyo sana kutoka kwa mhitimu huyo wa akademi ya klabu hiyo.
5. Brahim Diaz (Real Madrid)
Ushindi wa Real Madrid wa mabao 2-1 dhidi ya wapinzani wao wa jiji moja, Atletico Madrid ulikuwa ni pambano la mabao tukufu. Rodrygo alianza mambo kwa dakika nne tu kwa bao la kustaajabisha kwenye mguu wake 'dhaifu' zaidi, kabla ya Julian Alvarez kusawazisha.
Lakini alikuwa Brahim Diaz aliyefunga bao muhimu zaidi la mechi hiyo, akimtungua Jose Gimenez kwa ustadi kwenye kona ya mbali.
Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Morocco, ambaye alikuwa akiziba nafasi ya Jude Bellingham, amethibitisha kuwa naibu mzuri na hodari msimu huu na nguvu na wepesi wake ulikuwa muhimu katika ushindi wa Madrid.
4. Harry Kane (Bayern Munich)
Harry Kane amekosolewa mara kwa mara kwa kushindwa kujitokeza kwenye hafla kubwa, lakini hilo lilisawazishwa baada ya ushindi mnono wa Bayern Munich wa mabao 3-0 dhidi ya mabingwa watetezi wa Bundesliga, Bayer Leverkusen Jumatano.
Mechi baina ya timu hizi mbili zilikuwa zimetawaliwa na sare ya bila kufungana katika wiki kadhaa zilizopita, lakini ni Bayern ambao walikuwa wamekithiri katika hafla hii, kwa hisani ya mshambuliaji wao mkali wa England.
Kane alipanda juu ya Nordi Mukiele mapema katika harakati za kuipatia Die Roten bao la kuongoza wakati alipofunga kwa kichwa akiunganisha krosi kutoka winga ya kulia, kabla ya kushinda na kufunga penalti katika kipindi cha pili.
3. Wojciech Szczesny (Barcelona)
Wojciech Szczesny alianza maisha upya ya soka akitoka kustaafu akiwa Barcelona baada ya kusajiliwa kwa haraka kuchukua nafasi ya Marc-Andre ter Stegen aliyejeruhiwa. Safari ya mwisho ya raia huyo wa Poland dhidi ya Benfica ilikuwa mbaya kwani aliizawadia timu ya Lisbon mabao mawili katika pambano la ushindi wa 5-4 wakati wa awamu ya ligi.
Lakini Szczesny amekua na uhakika zaidi kila wiki inayopita na alipanda daraja Jumatano wakati Barcelona ya wachezaji 10 ikipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Benfica.
Kutolewa mapema kwa Pau Cubarsi kulifanya maisha kuwa magumu kwa wababe hao wa Katalunya, huku bao la Raphinha na ustadi wa Szczesny zikiwahakikikishia wanarejea nyumbani na faida.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, alikuwa mchezaji bora wa mechi katika Uwanja wa Da Luz baada ya kuokoa hatari nane.
2. Alisson (Liverpool)
Ukizungumzia kuhusu kiwango cha kufurahishwa basi muingize Alisson. Golikipa huyo wa Brazil alielezea umuhimu wake wakati wa ushindi wa Liverpool dhidi ya PSG kama "kiwango bora zaidi cha maisha yangu" na ni vigumu kumbishia kuhusu hilo.
PSG waliwatawala Liverpool katika kipindi kirefu cha mchezo wa Jumatano, lakini Alisson hakuweza kufungika. Mchezaji huyo mwenye umti wa miaka 32, aliokoa hatari tisa – ambazo zilionekana wazi kwamba zingeweza kuwa bao.
Khvicha Kvaratskhelia, Ousmane Dembele na Desire Doue wote mashuti yao yalikataliwa na kipa huyo.
1. Martin Odegaard (Arsenal)
Martin Odegaard amekuwa akishutumiwa kwamba haisaidii Arsenal wakati huu ambao imekumbwa na janga la majeruhi na nahodha huyo amecheza mechi nne bila bao au asisti. Lakini Odegaard alithibitisha thamani yake wakati walipoishushia mvua ya mabao PSV.
Odegaard alifunga mara mbili na kutoa asisti wakati Arsenal ilipokuwa ikifunga bila upinzani wowote.
Alikuwa katika kiwango bora zaidi kwa 'Washikabunduki' hao.
Kama Arsenal wataweza kupata medali yoyote msimu huu, basi ile ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ni bora zaidi kwao. Na kwa hilo, wanahitaji ubora wa aina yake kutoka kwa Odegaard.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED