Ulivyo mchakato mkunga anaumbwa, anakomaa akamkomboa mama, mtoto

By Yasmine Protace , Nipashe
Published at 04:50 PM Sep 25 2025
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Edward Mpogolo, akikabidhi msaada wa gari kwa wadau wa huduma za afya ya jamii, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Picha: Yasmine Protace
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam, Edward Mpogolo, akikabidhi msaada wa gari kwa wadau wa huduma za afya ya jamii, katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

INAPOTAMKWA mkunga, ina maana kitaalamu mtu anayehusika kuwahudumia kiafya wazazi wajawazito na vichanga vinavyozaliwa.

Mara zote inafafanuliwa kwamba, inabaki kuwa kielelezo cha utunzaji huduma za afya, kupanga na kumpatia mwanamke mhitaji, mkondo sahihi unaomfanikishia uzazi salama.

Ikiwa sehemu kubwa ya kundi hilo wataalam ni kinamama, elimu na mafunzo wanayopata wakunga inazama katika kumuunda awe mjuzi anayetambua hali na stadi za kumhudumia ama mjazito au mzazi wa kichanga, pia wote kwa pamoja.

Hivyo, wakunga wanapopata elimu bora ya masuala ya uzazi, wanatarajiwa kufanya kazi kwa weledi na kufanikisha kukabili shida iliyoko mbele yao.

Kimataifa, katika kulitambua hilo nchini, kuna harakati zinazoendana na majukumu ya ukunga, zikiangukia kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga nchini.

Hizo ni hatua zinazoanzia mifano kama ya ubia uliopo kati ya serikali na Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), wakijumuika na serikali ya Canada.

Hapo wakabidi huwa vifaa kazi, mavazi ya kujikinga wahudumu wa afya na magari mawili kwa washirika wa utekelezaji wa mradi uitwao “Thamani Uzazi Salama.” 

Mwakilishi Mkazi wa UNFPA nchini, Mark Schreiner, anasema katika makabidhiano ya vifaa hivyo, ananena:"Hii ni hatua muhimu inayoonesha mafanikio ya uwekezaji kwa watu."

Inatajwa kuwa namna ya kujenga mfumo wa afya thabiti wenye uzazi salama, kila mmoja anapata huduma bora inayoheshimika, ikifafanuliwa kuwa

fursa kusherehekea mavuno, wakunga wanapata mafunzo bora na yenye msaada kitaalamu.

Kwa mujibu wa mwakilishi huyo wa UNFPA, sasa jamii zina uelewa wa mila hizo kandamizi zinazopigwa vita, kukiwapo washiriki wa kiume katika afya ya uzazi.

"Mafanikio hayo ni matokeo ya ushirikiano thabiti, uwekezaji ulioratibiwa kwa dhamira ya pamoja ya kuokoa maisha," anasema Mark.

Anautaja Mradi wa Thamini Uzazi Salama wenye miaka saba sasa, ukitekelezwa na aasi za UNFPA, Amref Health Afrika, serikali ya Canada, pia Chama cha Wakunga Canada (CAM), ukilenga wakazi wa wilaya tatu mkoani Shinyanga.

Pia, kuna halmashauri tatu za mkoani Dar es Salaam, lengo likiwaendea wahitaji wa afya ya uzazi, mama mtoto na vijana, wakiongezewa idadi ya wakunga wajuzi, wanaoshirikiana na wadau wa ndani.

Balozi wa Canada nchini, Emily Burns, anasema taifa lake linajivunia kushirikiana na Tanzania kuwekeza katika wakunga na wahudumu wa afya, akiitafsiri:

“Ni kuwekeza katika utu, usawa kijinsia na mustakabali bora wa familia za Kitanzania. Magari yaliyokabidhiwa yataongeza ufanisi wa usimamizi, uratibu na huduma za uhamasishaji.

“Ni kuhakikisha kila jamii inafikiwa, ambako mradi huo unachangia malengo ya maendeleo endelevu na Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050 kwa kuimarisha mfumo wa afya kuanzia ngazi ya jamii," anasema.

Rais wa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA), Beatrice Mwilike, anataja kuwa siku pekee kwa Chama cha Wakunga Tanzania (TAMA), wakishuhudia hatua ya kuimarisha afya ya mama na mtoto kupitia Mradi wa Thamini Uzazi Salama.

Anautaja mradi kuwa kielelezo kinachohakikisha kila mjamzito anapata huduma salama ya kujifungua, kutoka kwa mkunga mtaalamu.

"Katika mradi huu... kwa mwaka huu tumeweza kufundisha wakunga 180 katika utoaji wa huduma za dharura kwa mama wajawazito na watoto wachanga 90 mkoani Dar es Salaam na 90 mkoani Shinyanga,” anasema.

Anaongeza kuwa vituo vilivyofikiwa mkoani Dar es Salaam ni hospitali nane, vituo vya afya 24 na zahanati 27 na kwa ujumla ni vituo 59.

Beatrice anaongeza kuwa eneo la pili, anatumia mifano mkoani Shinyanga, kuna jumla ya hospitali nne, vituo vya afya 22 na zahanati 46 jumla kukiwapo vituo.72.

Mdau huyo wa ukunga, anagusa matokeo ya mradi tajwa yamewajengea uwezo wakunga kukabiliana na dharura kubwa za uzazi, kama vile kutokwa na damu nyingi baada ya kujifungua.

Anaongeza kuwapo Uhusiano na Dira ya Taifa 2050 dhidi ya matokeo hayo, ni sehemu ya safari ya nchi kuelekea Dira ya Taifa ya 2050.

KAULI YA UONGOZI

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Jijini Dar es Salaam, Edward Mpogolo, aliyekuwa mgeni rasmi katika ugawaji vifaa hivyo, anasema kutolewa huko ni msaada kwa uzazi salama.

Anafafanua, wakunga waliofunzwa idadi yao sasa inazidi 3,000, mkuu wa wilaya akisema eneo lake hadi sasa kuna vituo nane vya afya vimejengwa, huku akihimza watendaji waandamizi kuwatumia wataalamu hao walionolewa.