Kiungo mkabaji wa Yanga, Khalid Aucho, ameweka wazi maisha yake binafsi kuwa hajaoa mpaka sasa, lakini anataka mwanamke ambaye atampenda kutoka moyoni na si kwa sababu ya pesa zake au umaarufu alionao.
Akizungumza na Nipashe Digital, akiwa na kikosi cha timu yake mazoezini, Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam, Aucho, ambaye ameanza mazoezi baada ya kutoka kwenye majeraha, akikosekama kwenye michezo kadhaa ambayo timu yake imecheza, alisema anatamani kuoa, lakini hajui ataoa lini kwani anachotaka yeye atokee mwanamke anayempenda, hapo na yeye ataweka mapenzi yake kwake.
Aucho pia amesema hajui ataoa wapi kama Tanzania au Uganda, ingawa nchi yoyote ile kati ya hizo kama atatokea mwanamke mwenye sifa anazozitaka, atafanya maamuzi.
"Sitaki mwanamke atakayenipenda kwa sababu ya umaarufu au pesa zangu, anipende kutoka moyoni kwa roho moja.
Kwa sasa sina mwanamke, niko singo, ila nina mtoto, mpaka sasa bado sijajua nitaona lini. Kwanza kabisa nataka nipate mwanamke mzuri sana na sijui kama nitampata Uganda au Tanzania, nataka mwanamke ambaye atanipenda kama mimi, siyo kwa sababu ni Aucho, au nina pesa, kama atanipenda kutoka moyoni, basi na mimi nitampenda pia, pesa za kuoa ninazo wala haina shaka," amesema Aucho.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED