Mauritania ilivyomaliza ukame CHAN

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 12:30 PM Aug 12 2025
news
Picha Mtandao
Mchezaji wa timu ya Mauritania, Ahmed Mokhtar Ahmed.

MFUNGAJI wa bao la Mauritania, Ahmed Mokhtar Ahmed, dhidi ya Jamhuri ya Kati, amesema ulikuwa usiku wa dhahabu kwake kumaliza ukame wa mabao kwa timu hiyo kwenye michuano ya CHAN.

Alikua tegemeo wakati Mauritania ikipambana kufuzu kwa michuano hiyo, na bao lake likaisaidia timu hiyo kuwa kwenye nafasi nzuri ya kufuzu robo fainali.

Katika michezo miwili, washambuliaji wa Mauritania walikuwa wametafuta mabao bila mafanikio, wakikosa dhidi ya Madagascar na Taifa Stars. 

Lakini Jumamosi, Mokhtar alibadilisha hadithi ndani ya dakika tisa baada ya kuanza kwa mechi na bao lililodumu hadi mwisho wa mchezo.

"Ninawapongeza wachezaji wenzangu na pia kocha baada ya ushindi dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati. 

“Sasa tumeshinda mechi yetu ya kwanza kwenye CHAN, na tutatazamia kutoa matokeo bora katika mechi yetu ijayo, Mungu akipenda," alisema El Moctar.

Ushindi huo wa bao 1-0 uliifanya Mauritania kufikisha pointi nne katika Kundi B na kuweka mlango wazi wa kufuzu hatua ya mtoano.