Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali itahakikisha inatekeleza masuala yote yaliyoanzishwa na aliyekuwa Spika wa Bunge, Hayati Job Ndugai, ikiwemo kuendeleza jitihada za kuitangaza Kongwa kama kielelezo cha makumbusho ya kupigania uhuru kwa nchi za Kusini mwa Afrika.
Majaliwa ametoa kauli hiyo leo, Agosti 11, 2025, wakati wa kutoa salamu za rambirambi kwa waombolezaji waliohudhuria mazishi ya Hayati Ndugai aliyefariki Agosti 6, mwaka huu jijini Dodoma.
“Wakati jana Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan akiongoza waombolezaji kutoa heshima za mwisho katika viwanja vya Bunge, aliagiza kukamilishwa kwa masuala yote yaliyoanzishwa na marehemu, ikiwemo agizo kwa mamlaka husika kuendeleza kuitangaza Kongwa kama kielelezo cha makumbusho ya kupigania uhuru kwa nchi za Kusini mwa Afrika.
“Napenda kuwahakikishia wananchi wa Kongwa kuwa tutasimamia agizo hili na kuhakikisha Serikali inatekeleza maagizo yote ya Rais kwa ukamilifu,” amesema Majaliwa.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED