MAWAKALA wa VinÃcius Júnior wameiarifu Real Madrid kuhusu mahitaji ya mshahara wa mteja wao kama ataendelea na klabu hiyo baada ya mwaka 2027, kwa mujibu wa chanzo cha ESPN.
Wawakilishi wa mchezaji huyo wana matumaini ya kukutana na viongozi wa Madrid katika siku zijazo ili kuendelea na majadiliano.
Kwa mujibu wa chanzo hicho, VinÃcius anakaribia kurefusha mkataba wake huko Madrid kuliko kuhamia Saudi Arabia, kama inavyoripotiwa kwenye vyombo vya habari vya Hispania.
Ligi ya Saudi Arabia inataka kumfanya fowadi huyo wa Brazil kuwa mchezaji anayelipwa fedha nyingi zaidi duniani, lakini vyanzo viliongeza kuwa tangu Desemba hakujakuwa na taarifa zozote kuhusu uhamisho huo.
Ingawa chanzo hakikufichua mahitaji maalum ya kifedha ya VinÃcius kubaki Madrid, lakini imaaminiwa kwamba mchezaji huyo anataka mshahara mkubwa zaidi ya Kylian Mbappé na Jude Bellingham.
Mkataba wa sasa wa VinÃcius unamalizika mwaka 2027 na kama ESPN ilivyoripoti hapo awali, mshahara wa mchezaji huyo unakaribia euro milioni 10 kwa msimu pamoja na nyongeza.
ESPN iliripoti wiki iliyopita kwamba Madrid ilikuwa imekutana na wasaidizi wa VinÃcius kwa ajili ya kuanza mazungumzo ya kuongeza mkataba.
Chanzo hicho kinaongeza kuwa VinÃcius hana haraka ya kufanya hivyo licha ya kuzungumza hadharani kuhusu nia yake ya kuendelea kubakia Madrid kwa muda mrefu.
***
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED