Wachezaji wa kuchungwa Yanga vs Simba

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 03:15 PM Mar 03 2025
news
Picha: Mtandao
Wachezaji wa Simba.

Derby ya Kariakoo kati ya Yanga na Simba ni moja ya mechi kubwa zaidi nchini, ikijaa ushindani ndani ya uwanja na tambo kutoka kwa mashabiki wa timu hizo mbili za mtaa wa Kariakoo.

 Hapa ni nyota wa kutazama kwenye derby hii. 

🔥 Kibu Denis

Tangu ajiunge na Simba, Kibu amekuwa mwiba hasa kwenye mechi za watani wa jadi. Katika derby alizocheza, amefanikiwa kufunga mabao mawili. Katika mchezo wa mwisho, alichezewa faulo nyingi kuliko mchezaji yeyote uwanjani.

Pacome ZouZoua

Mmoja wa wachezaji hatari anapopata nafasi ya kushambulia. Mikimbio yake na uwezo wa kupunguza wachezaji zaidi ya mmoja huleta tishio langoni kwa wapinzani.

🎯 Elie Mpanzu

Hii itakuwa derby yake ya kwanza tangu ajiunge na Simba dirisha dogo. Ameonyesha uwezo mkubwa na anatarajiwa kuwa mwiba kwa wapinzani kutokana na uwezo wake wa kupandisha mashambulizi.

Max Nzengeli

Tayari ameshafunga bao katika mechi za watani wa jadi. Uchezaji wake umekuwa bora sana, na anatarajiwa kuwa miongoni mwa wachezaji hatari katika mchezo huu.

🔥 Prince Dube

Hajacheza derby nyingi, lakini ni mchezaji mwenye rekodi nzuri ya kufunga dhidi ya Simba, akiwa amewafunga alipokuwa Azam FC. Anaweza kuleta tofauti katika mchezo huu.

Desse Mukwala

Si mchezaji anayeimbwa sana, lakini ana uwezo mkubwa. Kasi yake na pressing zinaweza kuleta kitu tofauti. Katika derby yake ya kwanza hakufunga, lakini alionekana kuwa tishio kubwa.

🎨 Stephane Aziz Ki

Kipaji kikubwa na mchezaji muhimu wa kuichezesha timu. Uwezo wake wa kupiga mashuti na kutoa pasi za mwisho unamfanya kuwa hatari anapokaribia eneo la 18 la mpinzani.

🔥 Charles Ahoua

Si mchezaji anayezungumziwa sana, lakini ni hatari katika mipira iliyokufa. Anaweza kuadhibu wapinzani au kusababisha timu yake kuadhibiwa.

Lionel Ateba

Katika derby yake ya kwanza, alikosa nafasi ya wazi ambayo ingeweza kumweka kwenye rekodi ya wafungaji wa mechi za watani wa jadi. Uwezo wake wa kusimama na mabeki zaidi ya wawili unaweza kufungua mianya kwa wachezaji wenzake.

🔜 #DerbyYaKariakoo | #YangaVsSimba | #NBCPL

✍🏽 Mwakalobo Jnr.