Gereza la Maweni lapongezwa juhudi matumizi nishati safi ya kupikia

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 09:26 AM May 13 2025
Gereza la Maweni lapongezwa juhudi matumizi nishati safi ya kupikia
Picha: Mpigapicha Wetu
Gereza la Maweni lapongezwa juhudi matumizi nishati safi ya kupikia

Bodi ya Nishati Vijijini (REB) imerishishwa na juhudi zilizochukuliwa na Magereza mkoa wa Tanga kwa kuanza kutumia Nishati Safi ya Kupikia katika kuandaa chakula cha Wafungwa wa zaidi ya 560 tofauti na hapo awali ambapo matumizi ya kuni na mkaa yalikuwa ni zaidi ya asilimia 100.

Akizungumza baada ya kutembelea Gereza la Maweni mkoani Tanga, Mei 13, 2025, Balozi Radhia Msuya amesema Bodi ya Nishati Vijijini (REB); imeridhishwa kwa kiwango kikubwa na hatua zilizochukuliwa Magereza mkoani humo katika kutekeleza agizo lililotolewa na Dk. Samia Suluhu Hassan, alilolitoa mwaka mmoja uliopita kuwa Taasisi zote zinazowahudumia watu zaidi ya 100 kuacha kutumia nishati chafu (Kuni na mkaa) ili kupunguza matumizi ya kuni na mkaa ambayo yanachangia uharibifu wa mazingira.

Baada ya kutembelea na kujionea miundombinu ya Nishati Safi ya Kupikia katika Gereza la Maweni mkoani Tanga Wajumbe hao wa Bodi ni pamoja na Wakili, Mwantum Sultan na James Mabula wamesema wameridhishwa kwa hatua zilizochukuliwa na Taasisi hiyo na kuongeza kuwa juhudi hizo, zitasaidia kufikia lengo la agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ambapo Magereza Tanzania Bara itapata shilingi bilioni 35 kama ruzuku kutoka Serikalini kupitia REA ili kutekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Nishati Safi ya Kupikia.

Kwa upande wake, Mkuu wa Magereza mkoa wa Tanga, ACP, Fredrick Massawe amesema  Magereza imejiwekea malengo endelevu ya matumizi ya Nishati Safi huku akishukuru ushirikino uliopo baina yao na REA ambao utawezesha Magereza kupata majiko banifu, mitungi ya gesi ya LPG, upatikani wa mkaa banifu (Rafiki Briquettes) pamoja na ununuzi wa mashine 61 za kutengeneza mkaa mbadala pamoja na kukuza uwezo kwa Watumishi 280 wa Magereza kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Naye Meneja Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi ya Nishati Safi, Mhandisi, Emmanuel Yesaya kutoka REA amesema, Septemba 13 mwaka jana REA ilisaini mkataba na Magereza ambapo Serikali itatoa ruzuku kwa ajili ya kuwezesha uboreshaji wa miundombinu ya Nishati Safi ya kupikia kwa Magereza yote Tanzania Bara ambapo utekelezaji ukaanza mwezi Desemba, 2025 na uda wa utekelezaji wa mradi huo utakuwa miezi 36 huku gharama ya Mradi itakuwa shilingi bilioni 35.

“Mradi huu unatekelezwa kwa awamu tatu zitakazohusisha; Ujenzi wa miundombinu ya gesi asilia katika Gereza la Lilungu Mtwara, ujenzi wa miundombinu ya mitambo 126 ya biogas, ujenzi wa miundombinu 64 ya gesi ya LPG, usambazaji wa mitungi ya gesi 15,558 ya kilo 15 pamoja na majiko ya gesi ya ‘plate’ mbili kwa Watumishi wa Magereza, usambazaji wa mkaa mbadala (Rafiki briquettes) tani 850, ununuzi wa mashine 61 za kutengeneza mkaa mbadala pamoja na kukuza uwezo kwa Watumishi 280 wa Magereza kuhusu matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia”. amekaririwa, Mhandisi, Yesaya.