Samia awapongeza wananchi Mtwara matumizi mazuri ya pembejeo za ruzuku

By Romana Mallya , Nipashe
Published at 10:12 PM Sep 23 2025
Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan
Picha: Mpigapicha Wetu
Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan

Mgombea urais wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan, amewapongeza wananchi wa Mtwara kwa matumizi mazuri ya mbolea na pembejeo za ruzuku.

Amesema korosho imetoka tani 15,000 hadi 24,000, ambapo mara ya mwisho iliingiza Sh. bilioni 73.

“Karanga uzalishaji umepanda toka tani 26,100 zenye thamani ya Sh. bilioni 65 hadi tani 33,170 thamani ya Sh. bilioni 82.9 zimeingia mikononi mwa wakulima.

“Ufuta uzalishaji umepanda kutoka tani 1580 zenye thamani ya Sh. bilioni 3.9 na kuvuka lengo la uzalishaji hadi tani 11800 zenye thamani ya Sh. Bilioni 38.8,” amesema.

Kadhalika ameahidi kwenda kukamilisha miradi ya visima na skimu za umwagiliaji maji na mabwawa, ili wakulima waendelee kunufaika na mazao wanayozalisha kwa kulima mara mbili kwa mwaka.

Ametoa ahadi hiyo leo Septemba 2025, wakati akizungumza na wananchi wa Mtwara akianza ziara ya kampeni mkoani humo.