Rais Samia Suluhu Hassan ameipongeza Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) kwa kuendelea kuboresha mifumo ya utatuzi wa Migogoro ya kikazi Kwa watumishi wa umma na sekta binafsi.
Aidha, amesema kwa upande wa sekta binafsi, Serikali ipo hatua za mwisho za kukamilisha mfumo wa usimamizi wa wa Migogoro kidijitali ambayo itawaondolea upotezaji muda na gharama katika ufuatiliaji wa mashauri yao.
Rais Samia ameyasema hayo jana Mei 1, 2025 akitoa Hotuba kwa wananchi katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi) yaliyofanyika kitaifa Mkoani Singida.
"Kwa Upande wa Shirika la Kazi Duniani (ILO), imeendelea kushirikiana na Mahakama ya Kazi, (NESCO) na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) Kwa utatuzi wa Migogoro ya kikazi Ili Kuboresha mahusiano bora kazini" amesema Rais Samia.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED