Taarifa za EWURA ni kioo cha kujipima na kujitathmini-Biteko

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 08:59 AM Apr 10 2025
Taarifa za EWURA ni kioo cha kujipima na kujitathmini-Biteko

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko, ameipongeza Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) kwa kuandaa Taarifa za Maendeleo ya Sekta ya Nishati( umeme, petroli na gesi asilia ) nchini, na kuleza kuwa taarifa hizo ni kioo cha kujipima na kutathmini ufanisi wa utendaji wa sekta hiyo katika kuwahudumia wananchi na watoa huduma.

Dk Biteko ametoa pongezi hizo wakati wa hafla ya kuzindua taarifa hizo, iliyofanyika jijjni Dodoma, Aprilli 09, 2025. 

Aidha, amewaasa  wananchi kuzisoma kwa kina taarifa hizo ili kubaini changamoto na fursa na zinazopatikana katika sekta ya nishati sanjari na hatua zilizochukuliwa na serikali kutafuta suluhu ya changamoto husika.