Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema katika kuimarisha udhibiti na kuzuia utoroshaji wa madini ya tanzanite, katika mwaka ujao wa fedha Wizara kupitia Tume ya Madini inakusudia kuja na mfumo na utaratibu thabiti ambao utawataka wakaguzi na wathamini wa madini hayo kuvaa kofia ngumu zenye kamera wakati wakitekeleza majukumu yao.
Akiwasilisha leo bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2025/26, Mavunde amesema lengo ni kurahisisha usimamizi na ufuatiliaji wa mwenendo kwenye eneo Tengefu la Mirerani na masoko kunakofanyika biashara ya madini hayo.
Aidha, amesema kutokana na mafanikio yatakayopatikana, utaratibu huo utatumika kwenye madini mengine ya vito.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED