WANACHAMA wa vikundi vya mfuko wa kuhifadhi Bahari 'MKUBA' kupitia kampeni ya ‘Bahari yetu Maisha yetu’, Kata ya Kwale, Kijiji cha Kichalikani, wilayani Mkinga, leo Aprili 16, 2025, wamekabidhiwa Sh. 13,000,000 kwa ajili ya kujikwamua kiuchumi kupitia mfumo wa kukopeshana wao kwa wao.
Fedha hizo zimetolewa na Shirika la Mwambao Coastal Community Network Tanzania, chini ya Ufadhili wa Blue Action Fund, unalenga kutoa Elimu ya Utunzaji wa Mazingira pamoja na kuwainua kiuchumi wakazi wa Mwambao wa Bahari, ili kupunguza utegemezi wa shughuli za kiuchumi baharini.
Akikabidhi fedha hizo kwa vikundi saba, vyenye wanachama zaidi ya 210, kati yao wanawake 167 na wanaume 43, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Amani Kasinya, amewashukuru wadau hao wa maendeleo kwa kuunga mkono jitihada za serikali za Utunzaji wa Mazingira ya Bahari, pamoja na kuinua uchumi kwa wakazi wa Mwambao wa Bahari,
Amani, amewataka wanufaika wa fedha hizo kuzitumia kwa malengo yaliyokusudiwa na wafadhili hao,
"Nawaomba wanufaika wa fedha hizi,mzitumie kwenye malengo yaliyokusudiwa na wafadhili wetu,msije mkaenda kufanya anasa,kumbukeni kuwa fedha hizi zimetolewa, ili mjikwamue kiuchumi," ameongeza Amani
Mkuu wa Uchumi na Uwezeshaji, kutoka Shirika la Mwambao Coastal Community Network Tanzania, Abubakary Masoud, amesema fedha hizo zimetolewa kwa dhamira kuu ya kutunza Bahari na Rasilimali zake kwa kuhakikisha matumbawe yanakuwa salama pamoja na viumbe wake pia kuzuia uvuvi haramu,
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED