Ofisa wa jeshi, mkewe, mlinzi wake wamo vifo sita ajali ya ndege

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 02:16 PM Aug 17 2025
Ajali imetokea takriban kilomita 34 kutoka Kisangani
Picha: CONGO RASSURE
Ajali imetokea takriban kilomita 34 kutoka Kisangani

WATU sita, pamoja na ofisa mmoja wa jeshi la DRC, FARDC, mke wake na mlinzi wake, wamefariki dunia katika ajali ya ndege Jumamosi, Agosti 16, takriban kilomita 34 kutoka Kisangani, katika mkoa wa Tshopo, DRC.

Kulingana na vyanzo vya usalama, vikinukuliwa na Radio OKAPI, mmoja wa abiria saba waliokuwamo amenusurika, ingawa ndege hiyo imeharibika vibaya kabisa.

Vyanzo hivyo vinaripoti kuwa mazingira ya mkasa huu bado hayajajulikana.

Oktoba mwaka jana, wanajeshi wawili walifariki na mmoja alinusurika katika ajali ya helikopta ya kijeshi kwenye uwanja wa ndege wa Ndolo, mjini Kinshasa.

Ndege hiyo ilianguka kwenye njia ya kurukia ndege katika uwanja wa ndege wa Ndolo. Mazingira ya ajali hiyo bado hayajafahamika.

Ndege hiyo ilikuwa ikitoka Lubutu, mkoani Maniema, kuelekea Kisangani. 

Vyanzo vya habari vya kijeshi vimethibitisha kuwa ndege hiyo ilikuwa imesimama Lubutu kwa miezi kadhaa. 

Ilikuwa safari yake ya kwanza na iliishia kwa kugonga mti.

RFI