Mtangazaji wa TV kutoka Marekani Tucker Carlson ametoa mahojiano yake na Rais wa Iran Masoud Pezzekian. Siku mbili zilizopita, alitoa video akisema kwamba alikuwa amemhoji Pezzekian na angeitoa hivi karibuni.
Pezzekian alimwambia mtangazaji huyo mashuhuri kwamba Israel ilijaribu "kumuua" alipokuwa kwenye mkutano.
Pia alisema kiongozi huyo wa Iran "anaamini hakuna kikwazo kwa uwekezaji wa Marekani nchini Iran."
Akijibu swali la Carlsen, "Je, serikali ya Israel imejaribu kumuua Rais wa Iran?", Pezzekian alisema, "Ndiyo, walijaribu, walijaribu kwa umakini. Lakini walishindwa."
Tucker Carlsen kisha akauliza, "Ikizingatiwa kwamba [Waisraeli] hawajawahi kuthibitisha hili popote, una uhakika walitaka "kukuua?" Pezzekian alijibu kwa kusema kwamba ni Israel ambayo "ilijaribu na kuchukua hatua" kumuua, si Marekani.
Aliongeza kuwa katika juhudi zao, “Nilikuwa kwenye kikao na tulikuwa tunajadili nini cha kufanya.
Kulingana na Pezzekian, "walishambulia kwa bomu mahali hapo kwa kutegemea habari waliyokuwa nayo kutoka kwa wapelelezi wao. Lakini Mungu asipotaka, hakuna kinachotokea." Hakutoa maelezo zaid.
Hapo awali, Ali Larijani, mshauri wa Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu na mjumbe wa Baraza la Kupambanua Mafanikio, alisema kuwa Israel "iligundua" eneo la mkutano wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa na kutaka "kuwaangamiza viongozi kwa kuwashambulia kwa mabomu, lakini hawakufanikiwa."
Rais wa Iran alisema: "Siogopi kuuawa nikitetea nchi yangu na uhuru. Lakini je, hii italeta utulivu?"
Tucker Carlsen kisha akauliza, "Kumekuwa na utulivu katika vita na Marekani. Unafikiri hili litatatuliwa vipi na ungependa likomeshwe vipi?"
Pezzekian alisema kuwa Iran haikuanzisha vita na "hatutaki vita kuendelea." Bw. Pezzekian alisema: “Tangu kuanza kwa kazi ya serikali, kauli mbiu yetu imekuwa daima kudumisha amani na nchi za eneo hilo.
Chanzo: BBC Swahili
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED