Elon Musk asema Marekani haina demokrasia tena

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 11:44 AM Jul 08 2025
Elon Musk
Picha: Mtandao
Elon Musk

Bilionea tajiri zaidi duniani, Elon Musk, ametangaza kuanzisha chama chake kipya cha siasa, akikiita "The America Party." Hatua hii inakuja wiki chache tu baada ya kutofautiana vikali na Rais wa Marekani, Donald Trump.

Katika mzozo huo, Musk aliweka kura ya maoni kwenye X akiuliza watumiaji kama kunapaswa kuwa na chama kipya cha siasa nchini Marekani.

Akirejelea kura hiyo ya maoni katika chapisho lake la Julai 5, 2025, Musk aliandika: "Kwa uwiano wa 2 kwa 1, mnataka chama kipya cha siasa na mtakipata! Linapokuja suala la kufilisisha nchi yetu kwa matumizi mabaya na rushwa, tunaishi katika mfumo wa chama kimoja, sio demokrasia. Leo, Chama cha America kimeundwa kukurejeshea uhuru wako." Ikisubiriwa utaratibu wa kisheria angalau ametangaza uwepo wake kwa umma.

Musk alitangaza kupitia jukwaa lake la mitandao ya kijamii la X kwamba ameanzisha chama hicho, akikiweka kama changamoto kwa mfumo wa vyama viwili vya Republican na Democratic nchini Marekani.

Dira yake ni kuvutia Wamarekani walioko katikati ya msimamo wa kisiasa, wale wasioridhika na Democrats au Republicans. Hii ni hatua ya kihistoria kutoka kwa bilionea huyo ambaye tayari ana ushawishi mkubwa katika sekta za teknolojia na mawasiliano.

Hata hivyo, kuingia rasmi kwenye siasa kunaambatana na changamoto nyingi. Makala hii inaangazia changamoto 8 kubwa zinazoweza kukikabili chama hicho katika safari yake ya kujikita kwenye mfumo wa kisiasa wa Marekani.

Chanzo: BBC Swahili