Waziri wa Mambo ya Nje wa Cyprus kuzuru Tanzania kuimarisha ushirikiano na EU

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 01:28 PM Jul 08 2025
Waziri wa Mambo ya Nje wa Cyprus, Dk.  Constantinos Kombos.
Picha: Mtandao
Waziri wa Mambo ya Nje wa Cyprus, Dk. Constantinos Kombos.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Cyprus, Dk. Constantinos Kombos anatarajiwa kufanya ziara nchini leo hadi Alhamisi kwa niaba ya Mwakilishi Mkuu wa Masuala ya Kigeni na Sera ya Usalama wa Umoja wa Ulaya ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Tume ya Ulaya, Kaja Kallas.

Lengo kuu la ziara hiyo ni kuimarisha mahusiano ya pande mbili, maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na ushirikiano wa kiuchumi chini ya mkakati wa Umoja wa Ulaya wa Global Gateway.

Balozi wa Umoja wa Ulaya kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Christine Grau, alipokuwa akizungumzia ziara hiyo, alieleza kuwa Tanzania ni mshirika wa kuaminika na mwenye utulivu katika eneo lenye umuhimu wa kimkakati.

Ziara hii ni matokeo ya uhusiano mzuri wa kidiplomasia kati ya Serikali ya Tanzania chini ya uongozi wa Rais Samia na Umoja wa Ulaya, pamoja na uongozi wake bora ambao umevutia mataifa na mashirika ya kikanda.