Tabasamu limerejea kwa wakazi wa Ilala mkoani Dar es Salaam baada ya Mkuu wao wa Wilaya Edward Mpogolo kuzindua utoaji wa mikopo ya asilimia kumi huku ikiwa tayari Sh bilioni 18 zimetengwa kwaajili hiyo.
Mpogolo hivi karibuni anapozindua kuanza kwa utolewaji wa mikopo hivi karibuni katika wilaya yake anasisitiza hakuna takayekosa mkopo na kwamba yupo tayari kushirikiana na viongozi wengine kushuka chini kutoa elimu kwa waombaji ili wasikose sifa.
Kwa muujibu wa maelezo yake Mpogolo fedha hiyo inagusa makundi ya wanawake, vinjana na watu wenye ulemavu na tayari vikundi 945 vimewasilisha maombi.
Katika ufafanuzi wa hilo, anaanza kwa kupongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya kwa kushirikiana na viongozi wake wa chini kuimarisha makusanyo akikumbushia katika kipindi cha miaka minne halmashauri hiyo ilikuwa inakusanya kwa mwaka Sh bilioni 61 lakini sasa inakusanya Sh bilioni 130.
Anasema makusanyo hayo yameongeza mara mbili ya yale yaliyokuw yanakusanywa kipindi cha nyuma na kwamba si jambo lilikuja kwa bahati mbaya bali ni matokeo ya juhudi za Mabelya na viongozi wengine katika kukusanya mapato.
Anasema kutokana na makusanyo hayo kuongezeka wanakwenda kutoa mkopo wa Sh bilioni 18.3 na kwamba kama wangelega katika ukusanyaji wa mapato hata mkopo huo ungekuwa kidogo.
“Ninakishukuru Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa na uongozi ambao mara zote umekuwa ikisistiza kuhusu kuanza kwa utolewaji wa mikopo hiyo tunawashukuru kwa usimamizi wenu pamoja na benki za CRDB na NMB kwa kulipokea jukumu la kutoa mikopo.
“Leo hii kwetu Wanailala ni fahari, tafrija na mwanzo mpya wa kutekeleza maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuanza kutoa mikopo kwa mfumo jumuishi kwa kushirikiana na benki.
“Sisi ni moja ya Halamshauri ya mfano kwa sasa lazima tufanye vizuri ili nyingine ziige kutoka kwetu vikundi ambavyo vimeomba mkopo ni zaidi 945 na katika hivyo 613 ni akina mama na wadada
Huko ndio unakuta magenge, biashara wanatengeneza vitu mbalimbali, vikundi vya vijana viko 310 na watu wenye uhitaji maalumu vipo vikundi 22 vyote hivyo vimedhamiria kuomba mkopo wa Sh bilioni 50.3 mana yake dhamira ya kumuunga mkono Rais ni kubwa kuliko uwezo wa kutoa mikopo” anasema Mpogolo huku akiwasisitiza watakao pata fedha wakumbuke kurejesha ili kuepuka mgogoro na serikali
Mpogolo anavitaka vikundi vilinavyo omba mkopo na vyenye nia kujitokeza katika mafunzo yatakayo wasaidia kutatua changamoto mbalimbali zitakazo wafanya waweze kuiomba na kurejesha madeni.
CHANGAMOTO
Katika ufafanuzi wake wakati wa kuzindua mikopo hiyo katika viwanja vya Karimjee Dar es Salaam Mpogolo anasema zipo changamoto tatu ambazo huchangia kukwama kwa huduma hiyo.
Anasema changamoto ya kwanza ipo kwa wasimamizi wa mikopo hiyo, ya pili ipo kwa wakopaji na ya tatu masuala ya elimu.
“Unakuta yuko mtu anaomba mkopo wa Sh. milioni 60 halafu mradi wake anapika chipsi ukimuuliza utafanyaje marejesho anasema we nipe kwanza uone nitakavyo rejesha.
“Yupo mwingine nafanya biashara ya kushona nguo ili apate fedha nyingi anaenda kumtafuta mwenzake mwenye shule ya ‘nursery’ ili aombee mkopo baadaye wagawane yeye apeleke huko na yeye aende kwenye vitambaa.
“Baadala ya kuomba cherehani, mashine ya kudarizi meza ya biashara anaenda kuomba kupitia shule akiulizwa atarejeshaje anakupeleka kule kwenye mashine ya kudarizi sasa Sh milioni 500 kwa mashine ya kudarizi atalipaje?
“Yupo mwingine anaomba mkopo kwa Mkurugenzi kwamba anapeleka mchele baharini…wapo mabaharia kule anaulizwa utarudishaje hiyo fedha anasema si unaona haka kagenge hapa?... nauzaga samaki sasa akijitahidi kumsaidia anaona ile hesabu ya samamki haiwezi kurejesha milioni 300 kwahiyo anamwambia fikiria tena.
“Yupo mwingine anaomba mkopo unamwambia twende tukakukague biashara yako anakwambia anafanyia mtandaoni ‘online’ ukimuuliza utalipaje mkopo ukinikimbia nitakukuta wapi? anasema tutakutana mtandaoni simu yangu imesajiliwa.
“Lakini ukifutilia utakuta ana genge lake anauza chakula sasa unamwambia kwanini usiombee biashara hii huo mkopo kuliko kusema hiyo ya mtandaoni ili tukusidie? hana majibu” anasema mpogolo anapowasilisha changamoto wanazokutana nazo
Anasema Changamoto nyingine wapo wanaoitwa kwa mkumbo kuingia kwenye mkopo unakuta mtu amekusanya watu akishapata mkopo anawagawia mwingine milioni mbili, mwingine moja baadaye wakihojiwa wanasema waliitwa tu kwahiyo mambo kama hayo yanapelekea wengi wao kushindwa kupata mikopo.
Aliwaonya akina mama hao kutodanganyika na wanaowashawishi kuomba fedha nyingi kama milioni 40 na kwamba itakuwa vigumu wanapotakiwa kutoa maelezo ya namna watakavyo zirejesha.
“Wasiwadanganye wengine wanashawishiwa omba Sh milioni 40, sasa ukiomba hiyo wakati unatakiwa kutoa maleezo namna gani utailipa kwa sababu ulikuwa hujajiandaa huwezi kusema au kutoa maelezo ya kushawishi upate mkopo.
“Lakini ukienda karume kwa mama ntilie atajua mchele anapataje unga anapataje anuza sahani ngapi ukimuuliza huyu maswalia anakujibu ukienda kwa mama anayeuza batiki atakujibu” anasema Mpogolo ambaye pia ni mlezi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
Anataja changamoto ya tatu ni elimu ya namna ya kuingia katika mfumo na kuomba mkopo kwa kutumia kompyua.
Katika hilo anasema tayari wameshakubaliana na mkurugenzi Mabyela kushuka chini na kuwafundisha wananchi namna ya kuingia kwenye mfumo na kujaza taarifa.
Anasema hawampimi Rais kwa fedha hiZo za mikopo pekee bali pia kwaajira zitakazo patikana baada ya watu hao kupata fedha hizo.
“Tunampima kwa makubwa aliyoyafanya kwa ajira zitakazo patikana kulingana na fedha hizo mama lishe wangapi wataajiri wasaidizi wangapi watanunua chelehani kwaajili ya kushona ajira itakayo zalia ndicho kipimo cha Rais kwetu.
“watu hapa mtapata fedha mtaweza kuhudumia familia maradhi yatapungua kwa sababu mtaweza kujihudumia, watu watakata bima za afya, ndoa zitadumu kwa sabbau wakati mwingien zinavunjika kwa umasikini na mapato ya halmashauri yataongezeka” anasema Mpogolo huku akishangiliwa na wanawake waliojitokeza katika uzinduzi
Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Rehema Sanga naye hayuko mbali na alicho kizungumza Mpogolo hapa anasisitiza watakaopata mkopo kufanya mapinduzi ya kweli katika kurejesha.
Anasema jukwaa lake linapendekeza mpango wa Pamoja wa Kukuza biashara kwa kuwafundisha wanufaika wa mikopo kwa pamoja.
Anasema jukwaa hilo liko tayari kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo Kutoa warsha kuhusu kuongeza faida, kufikia masoko na kutumia majiko safi ya kupikia.
“Kutumia mtindo "Mama wa Nguvu" wa ushauri na ufuatiliaji ili kuwe hakuna biashara itakayo filisika, Kuchuja vikundi, kutengeneza mipango ya biashara inayokubalika na taasisi za fedha, na kurahisisha mchakato wa kufuata vigezo.
“Kutambua wanawake wenye uwezo mkubwa kwenye kila Mtaa ili washiriki kwenye awamu inayofuata ya mikopo na kwamba ahadi ya jukwaa tumesimama imara kama jeshi la mashinani iliuhakikisha mikopo inalipwa kwa zaidi ya asilimia 95.
“Kupanua mikopo ya 10% ya Halmashauri kufikia wanawake 5,000 kufikia mwaka 2026, na Kuunganisha maajiko safi ya kupikia katika kila kifurushi cha mkopo” anasema rehema ambaye pia siku chache zilizopita alitunukiwa tuzo ya kutambuliwa kama mmoja ya viongozi wanao saidia wanawake kuinuka kiuchumi
WASEMAVYO WANUFAIKA
Mkazi wa Kitunda aliye jitambulisha kwa jina la Mama Godi, anasema mikopo hiyo itawavusha kutoka hatua moja kwenda nyingine kiuchumi.
Anasema yeye anajishughulisha na uuzaji wa samaki wabichi anatarajia kwenda kukopa fedha hizo ili akuze mtaji wake.
“Tunamshukuru Rais Samia na Mkuu wa Wilaya Mpogolo kwa sababu waliahidi na wametimiza kwa vitendo” anasema Mama Godi
Mkazi mwingine wa Segerea, Sophia Juma anasema walikuwa wanaisubiri mikopo hiyo kwa hamu na wamejipanga kufanya biashara zitakazo wasaidia kurejesha madeni ili waweze kupata nafasi ya kukopa tena.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED