Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na ACT Wazalendo vumelaani shambulio la kinyama dhidi ya Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dk. Charles Kitima, lililotokea usiku wa tarehe 30 Aprili 2025 katika makazi yake, Kurasini, Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Jeshi la Polisi na vyombo vya habari, Padre Kitima alivamiwa na watu wasiojulikana na kujeruhiwa.
Vyama hivyo vimesema shambulio hilo ni ishara ya njama za kuzima sauti za hoja na kueneza hofu kwa walioko mstari wa mbele kudai haki, uhuru na mageuzi ya kweli. Ni jambo lisilokubalika katika taifa linalozingatia misingi ya haki, amani na demokrasia.
Tunazitaka mamlaka husika zichukue hatua za haraka kuwabaini na kuwachukulia hatua wahusika wa tukio hili. Vilevile, Serikali itimize wajibu wake wa kulinda usalama wa viongozi wa dini, wanaharakati na wananchi wote, kwani vitendo vya uvamizi na watu kupotea vimeanza kuzoeleka kwa namna ya kutisha.
Aidha vyama hivyo kwa pamoja vimetoa pole kwa Padre Kitima, familia yake na Baraza la Maaskofu Katoliki kwa mshtuko na madhila yaliyotokea.na kuunganan nao katika kusisitiza haja ya kulinda misingi ya utu, usalama na uhuru wa kujieleza.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED