Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Wolfgang Pisa, amekanusha vikali taarifa iliyotolewa na jeshi la Polisi kuhusu kushambuliwa kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu (TEC) Dk. Charles Kitima na kudai polisi wanapotosha.
Askofu Pisa amesema kuwa si kweli kwamba katibu mkuu huyo alikua anapata kinywaji kabla ya kushambuliwa.
"Hakuna baa katika eneo aliloshambuliwa Fr. Kitima, hivyo hakuwa anapata kinywaji kama inavyoelezwa. Pale ni mgahawani. Kusema alikua anakunywa saa zote hizo si kweli. Tunaandaa taarifa kamili, tutaitoa itakapokua tayari"
Askofu Pisa anasema Dk. Kitima ameshambuliwa kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na kujeruhiwa kidevuni. Shambulio limefanyika alipotoka eneo la mgahawa ambalo hulitumia siku zote.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED