Mmoja mbaroni akidaiwa kumjeruhi Padre Kitima

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 08:46 AM May 01 2025
news
Picha: Mtandao
Kamanda Jumanne Murilo

Jeshi la Polisi limesema limepokea taarifa za kujeruhiwa kwa Katibu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC),Padri Charles Kitima kwa kushambuliwa na kitu butu kichwani na watu wawili wasiojulikana wakati akielekea maliwatoni.

Taarifa kwa umma iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, imeeleza kuwa Padri huyo inadaiwa tangu saa tatu asubuhi walikuwa na kikao na viongozi wa dini mbalimbali na baada ya kikao kuisha saa 1 jioni alikwenda kwenye kantini yao ambapo aliendelea kupata kinywaji hadi saa nne na robo alipokwenda maliwatoni pembeni ya kantini hiyo ndipo alidai kushambuliwa kichwani na kitu butu na watu wawili.

"Alipelekwa Hospitali ya Agakhan na anaendelea vizuri na matibabu. Mtu mmoja Rauli Mahabi @haraja mkazi wa Kurasini anashikiliwa na kuhojiwa kuhusiana na tukio hilo. Uchunguzi wa kina unaendelea ili hatua kali na za haraka zichulikuliwe kwa wahusika,"imefafanua taarifa hiyo.


Mapema alfajiri ya leo Mei mosi,2025 zilisambaa taarifa kwenye mitandao ya kijamii zikieleza kuwa Padri Kitime amejeruhiwa vibaya na watu wasiojulikana.

Endelea kufuatilia akaunti zetu tutakuketea kila kinachoendelea hapa....