Chama cha ACT Wazalendo kimelalamikia hatua ya Jeshi la Polisi na baadhi ya wakuu wa wilaya kuanza kuwasiliana na viongozi wa chama hicho wakitaka majina ya wagombea wa ubunge na udiwani, hatua waliyoitaja kuwa batili na ya kuvuruga mchakato wa uchaguzi.
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu akizungumza leo Julai 10, 2025 amesema kuwa maeneo ya Kilwa, Kigamboni, Kinondoni, Magu na Tarime yameripoti mawasiliano hayo, ambayo ni kinyume na sheria, kwani majina ya wagombea huwasilishwa tu kwa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC).
ACT Wazalendo imesema tayari imewasilisha malalamiko kwa IGP, Msajili wa Vyama vya Siasa na INEC, na kuwaelekeza viongozi wake kutotoa taarifa yoyote kwa Polisi kuhusu wagombea.
“Hatutaogopa. Tutaendelea kushiriki uchaguzi huku tukipigania haki, uwazi na uchaguzi wa kweli,” amesema Katibu Mkuu huyo.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED