Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika na Bodi ya Wadhamini wamemuandikia barua Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania ya kumtaka Jaji Hamidu Mwanga ajitoe kusikiliza kesi iliyofunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar, Said Issa Mohamed na wenzake.
Maombi hayo ya barua yanatarajiwa kusikilizwa Juni 14, 2025 saa nne asubuhi mbele ya Jaji Mwanga, pande zote mbili zitawasilisha hoja zao kuhusiana na maombi hayo ya CHADEMA.
Mbali na Mohammed, wengine ni Makamu Mwenyekiti Mstaafu wa chama hicho, Ahmed Rashid Khamis na Maulida Anna Komu wanaojitambulisha kama wajumbe wa bodi ya wadhamini
Wachama hao walifungua kesi mahakamani hapo wakidai kwamba Chama hicho, kimekuwa kikiitenga Zanzibar katika kuendesha shughuli zake ikiwemo suala la rasmali fedha.
Pia, wamedai kuwa kumekuwa na mgawanyo usio sawa wa mali za chama na rasilimali za kifedha kati ya Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara, pia wanadai kuna ubaguzi wa kidini na kijinsia.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED