Pata mapinduzi darasa, kinyesi cha binadamu dawa mpya ya tumbo

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 06:59 PM Jul 10 2025
Suala la usafi chooni limepiga hatua mpya, zao la chooni nalo limekuwa malighafi ya dawa
Picha: Mtandao
Suala la usafi chooni limepiga hatua mpya, zao la chooni nalo limekuwa malighafi ya dawa

NCHINI Uingereza madaktari wamebuni njia mpya ya kusafisha utumbo kukabiliana na wadudu sugu wanaojulikana kama ‘superbugs,’ wakitumia vidonge vyenye kinyesi kilichokaushwa kwa kugandishwa.

Utafiti huo mpya unalenga wagonjwa ambao wameambukizwa bakteria sugu ndani ya miezi sita iliyopita, wastani wake maana ya tangu mwaka 2015, kuanza.

Katika vipimo hivyo, kinyesi kinachukuliwa kutoka kwa wachangiaji wenye afya. Kila sampuli ya kinyesi inapimwa ili kuhakikisha haina bakteria hatari, chakula ambacho hakijameng'enywa huondolewa, kisha kinakaushwa kwa kugandishwa na kusagwa kuwa unga.

Unga huo huhifadhiwa kwenye tembe (kidonge) inayoweza kupita tumboni bila ya kuathirika na kufika kwenye utumbo. Huko inafunguka na kutoa unga huo kwenye kinyesi.

Inatajwa kuwa mpango mpya wa kupambana na vijidudu sugu ambavyo huua karibu watu milioni moja kila mwaka

UNDANI WA KINYESI

Sifa hiyo huanzia katika rangi zake, kila moja ikiwa na maana yake kitaalamu. Kinyesi huweza kuwa na rangi aina tofauti tofauti. Aina hizo hutokana na chakula ulichokula au ugonjwa fulani ndani ya mwili.

Inapokuwa na rangi ya kijani, huchukuliwa kama rangi za kawaida. Kuna aina chache za rangi ya kinyesi hushukiwa kwamba kuna kitu kulani mwilini hakiko sawa ama kuna ugonjwa ndani ya mwili unaotakiwa kutibiwa

Rangi ya kinyesi mara nyingi huathiriwa na kile mtu anakula, pia kiasi cha nyongo kilichotolewa na kibofu cha nyongo. 

Nyongo ni majimaji yenye rangi ya njano kuelekea kijani yanayotumika kumen’genya chakula chenye mafuta. 

Inapokuwa inasafiri kwenye utumbo, hubadilishwa na vimengenya vingine, hata ikabadilika rangi kutoka kijani kwenda kahawia. Kinyesi cha binadamu hupewa rangi yake asilia na nyongo.

Pale inapotokea kinyesi cha mtu kina rangi nyekundu, hapo inamaanisha kuwapo damu na kuna athari, hali inayomhimiza mgonjwa kumtafuta daktari kwa matibabu.

SIFA ZA RANGI

Rangi ya kijani inaweza kumaanisha kuwa chakula wakati kipo kwenye utumbo kilikuwa kinapita kwa kasi zaidi, mfano kwa sababu ya kuhara na kadhalika. 

Kupita kwa kasi hiyo husababisha nyongo kutopata muda wa kumen’genya chakula hicho ipasavyo na hivyo kutoka kama kilivyo au pasipo kumengenywa vema na nyongo. 

Chakula na dawa zinaelezwa kuweza kusababisha kinyesi kuwa na rangi ya kijani, vilevile hali inayopatikana kutoka boga za kijani kwa wingi, vyakula vyenye rangi ya kijani kama vyakula na vinywaji vyenye rangi ya kijani na vidonge vya madini chuma, hufanya mtu kupata kinyesi cha kijani.

Rangi mpauko au udongo: Hiyo huchangiwa na kukosekana nyongo katika kinyesi. Hiyo inaweza kumaanisha kuwa mirija inayopitisha nyongo imeziba. 

Mtu, pia anaweza kuwa na dalili nyingine ya manjano endapo mirija ya nyongo imeziba. Pia, kuna chakula au dawa zinazosababisha hali hiyo. 

Kuna dawa za kuzuia kuhara zinazosababisha mtu kuwa na kinyesi cha rangi hiyo. 

Rangi ya njano na ya utelezi au inayonuka kama mnyama aliyekufa: Kuwapo mafuta mengi katika kinyesi, huwa ni kwa sababu ya matatizo ya ufyonzaji chakula katika utumbo.

Vyakula vinvyochangia kusaabisha hali hiyo vinajumuisha protini aina ya ‘gluten’ inayopatikana kwenye vyakula kama mkate na nafaka. 

Mhusika anashauriwa kumuona daktari kwa vipimo zaidi endapo anapata choo cha namna hiyo kwa muda mrefu.

Rangi nyeusi: Hiyo huendana na kuvilia damu katika sehemu za mwanzo za utumbo kama vile kwenye utumbo mpana na utumbo mwembamba. Hali ya kuvia huweza kusababishwa na vidonda vya tumbo au majeraha ya ndani.

Pia, dawa au vyakula vinaweza kusababisha hali hiyo, vilevile dawa za kuongeza damu zenye madini chuma ama matunda meusi kama juisi ya zabibu au juisi yenye rangi nyeusi n.k

Kuna hali ya kula mkaa au udongo, na kunasababisha mtu kuwa na choo cheusi. Hata hivyo kinyesi chenye nyongo nyingi nacho kinaweza kuwa cheusi kwenye mwanga hafifu na kwenye mwanga mwingi, huonekana kuwa na rangi ya kijani inayoelekea nyeusi.

Kinyesi chekundu: Kuvia damu sehemu za mwisho za utumbo mdogo kama vile utumbo mpana na makalio huchagia.

Ufafanuzi huo, una dawa nazo zinazosababisha rangi hizo kama vyakula vyenye rangi nyekundu kama  nyanya na juisi, vimo katika orodha ya yanayochangia hali hiyo.

·        Makala hii ni kwa mujibu wa taarifa rasmi mbalimbali za kiafya.