Aripoti kazini akidhani kateuliwa na Rais Samia

By Mwandishi Wetu , Nipashe
Published at 05:38 PM Jul 02 2025
Rais Samia Suluhu Hassan.

Siku chache baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kumteua Shabani Kabelwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua mkoani Tabora;. Katika hali isiyokuwa ya kawaida mtumishi mmoja wa umma kutoka Mkoa wa Tanga ambaye majina yake mawili kati ya matatu yamefanana na mkurugenzi huyo amewahi kuripoti ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora kabla ya mteule wa Rais akidhani kwamba yeye ndio kateuliwa kwenye mkeka wa Rais kushika wadhifa huo.