Kazi ipo! ndivyo unavyoweza kueleza, baada ya leo Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara na Huduma Tanzania (UWAHUTA), Martin Massawe, kuchukua rasmi fomu kuomba kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM), kugombea Ubunge, Jimbo la Moshi vijijini.
Massawe, pia aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Kariakoo, Jijini Dar es Salaam hadi mwaka 2024.
Wakati anachukua fomu hiyo leo Julai 2, 2025 katika Ofisi za CCM, Wilaya ya kichama ya Moshi Vijijini, Massawe ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Wilaya.
Makada wengine waliochukua fomu hiyo hadi kufikia Julai 2, ni Mbunge wa sasa anayemaliza muda wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi aliyemaliza muda wake, Moris Makoi, Deogratius Mushi na Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA, aliyetimkia CCM, Felister Njau.
Wengine ni, Victor Tesha, Abdon Mallya, Vicent Massao, Salim Kikeke, Gloria Mushi, Wakili Wilhard Kitali na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Wilaya ya Moshi Vijijini, Theobald Mworia.
© 2025 IPPMEDIA.COM. ALL RIGHTS RESERVED